Breaking News

Nov 20, 2021

WATUMIA MAPATO YA MISITU KUJENGA NYUMBA YA MGANGA WA ZAHANATI KUNUSURU UHAI WA MAMA NA MTOTO

 

AFISA MTENDAJI KIJIJI CHA IHOMBWE, VASHTY CHIMILE AKIZUNGUMZA WAKATI WA KIKAO CHA PAMOJA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI KIJIJI CHA IHOMBWE MAMLAKA YA MJI MDOGO MIKUMI WILAYANI KILOSA

WATUMIA MAPATO YA MISITU KUJENGA NYUMBA YA MGANGA WA ZAHANATI KUNUSURU UHAI WA MAMA NA MTOTO

Na Lilian Lucas  

KIJIJI Cha Ihombwe kilichopo Mamlaka ya mji mdogo wa Mikumi Wilayani Kilosa mkoani hapa kimefanikiwa kutumia mapato ya misitu kujenga nyumba ya mganga wa zahanati ya kijiji na kunusuru uhai wa mama na mtoto kwa kuwapunguzia safari ya zaidi ya km 20 kufuata huduma ya afya Mikumi.

Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji wa kijiji Cha Ihombwe Vashty  Chimile wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Shirika la kuhifadhia misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa JAMII wa usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) juu ya maendeleo na changamoto za usimamizi shirikishi wa misitu kwa jamii (USMJ) kupitia mradi wa kuhifadhia misitukwa kuwezesha biashara endelevu ya misitu Tanzania (CoforEST) linalotekeleza mradi katika wilaya saba za Tanzania kupitia ufadhili wa Uswisi (SDC).

Jambo la Kutembelea umbali kwa akinamama kunasababisha kinamama kujifungulia njiani na wengine kuhofiwa kupoteza maisha.

Chimile alisema kabla ya mradi wa CoForEST ulioanzishwa mwaka 2019 jamii ikiwemo kinamama hasa wajawazito saba wajifungulia njiani kwa sababu walitumia muda mwingi barabarani kwenda hospitali ya Mtakatifu Kizito kupata huduma kwa sababu mganga wa zahanati alilazimika kwenda kijijini mara moja kwa wiki baada ya kukosa nyumba ya kulala.

 

WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI KIJIJI CHA IHOMBWE WILAYANI KILOSA, WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAAFISA KUTOKA MJUMITA NA TFCG

Alisema baada ya kuchoshwa na usumbufu huo na kuona wanayo makusanyo ya mapato ya mradi waliamua kutengwa kiasi fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mganga  wa zahanati, madarasa, kujenga vyoo 2 vya shule ya msingi Ihombwe, kuweka umeme kwenye majengo ya Serikali,  ukarabati wa barabara kwa kiwango cha changalawe fedha ambazo zilitokana na mapato ya mazao ya misitu ya zaidi ya shilingi milioni 200 walizokusanya tangu mradi unaanza hadi mwaka 2021.

Naye mmoja wa wajumbe ya kamati ya msitu wa kijiji. Asteria Maliki alisema wamama wamekuwa wahanga wakubwa wa changamoto za kiafya na kwamba anaushukuru mradi kwa kuwawezesha kupata pesa za kutosha za kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

"awali hatukuwa na nyumba ya mganga hapa na mama akishikwa uchungu usiku hulazimika kujifungulia njiani akienda ambako si salama, na wengine wamekuwa wakifariki njiani, ambao sina idadi yao" alisema.

No comments:

Post a Comment