KANALI SIMBAKALIA AUTAKA UONGOZI WA CHUO KIKUU MZUMBE KUFUATA NYAYO ZA MWALIMU NYERERE
Na Lilian Lucas
MKURUGENZI mstaafu wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje(EPZA) Kanali mstaafu Joseph Simbakalia ameutaka Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kusimamia kikamilifu yale yote yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwaeleza vijana wa sasa juu ya uadilifu wake,
Alisema hayo wakati wa kongamano la 17 la kumbukizi ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe lenye dhana ya Mtazamo wa Mwalimu Nyerere Juu ya Uchumi Mzunguko.
Kanali Simbakali alisema hayati Mwalimu Nyerere ambaye mchango wake katika Nyanja mbalimbali ameiachia Tanzania, Afrika na ulimwengu urithi wa kipekee, ni miongoni mwa viongozi wa kwanza walioshiriki kikamilifu kuleta uhuru wa bara la Afrika na hata kuanzisha harakati za kuliunganisha bara hilo.
“Kama maono, uadilifu na harakati za Nyerere zitaelezwa kwa kizazi cha sasa ni imani yangu kuwa chuo kitatoa wataalam waliobobea na mahiri katika uongozi, walio waadilifu na wanaoendana na mahitaji ya sasa ili waweze kushiriki moja kwa moja katika kuleta maendeleo ya watu,”alisema.
Aidha aliwataka vijana kujitahidi kupata maarifa sahihi ili kuweza kujenga uwezo wa kulisaidia taifa kuzidi kusonga mbele katika kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kuzingatia misingi ya uchumi mzunguko.
“Hapa wengine mtakuwa viongozi katika Serikali, mashirika ya umma nay ale binafsi niwasihi tu kuwa msiende kinyume na miiko ya taaluma zenu kwa kujihusisha na rushwa ambayo inalitia hasar taifa na kufanya wananchi na serikali yao kukosa amani,”alisema.
Wakati huo huo Kanali mstaafu Simbakalia alishauri Chuo Kikuu Mzumbe katika kujipambanua kipekee kuanzisha Shule ya Serikali ambayo itafahamika na kutambulika ulimwenguni kwa umahiri, utafiti wa masuala mtambuka, utawala bora na uchumi.
Kanali Simbakalia alisema kama chuo ambacho ni fuo la kuandaa viongozi bora wa kuwatumikia wananchi kwa weledi katika ngazi zote kuwepo kwa ‘Mzumbe School of Government, ni imani yake kuwa mijadala ya falsafa za Mwalimu Nyerere na utekelezaji ni muhimu kwa manuafaa ya watanzania hivyo maendeleo na ustawi wa jamii, uhusiano wa kimataifa na mengine yatasaidia kutambulika katika ulimwengu wa sasa kupitia shule hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka akizungumza katika kongamano hilo alisema kuwa chuo hicho kitahakikisha kinaendeleza na kuwafundisha vijana wanaojiunga chuoni hapo yale yote aliyoyahasisi Mwalimu Julius Nyerere kwa weledi ma na wao waweze kupata manufaa.
Profesa Kusiluka alisema katika kipindi cha
Nyerere mambo mbalimbali yaliweza kuanzishwa yaliyohusu kukuza uchumi na imani
ni kwamba vijana wa sasa wanatakiwa kufanya kazi kwa lengo la kukuza uchumi na
iwe lengo la kila kijana hasa aliyepata fursa ya kusoma chuo kikuu kuchangia
katika kuitoa nchi hii pale ilipo kwenda mbele.
No comments:
Post a Comment