VIJANA WENYE ULEMAVU WA AKILI NA FURSA KWENYE VITUO, VYUO VYA UFUNDI STADI
Na Lilian Lucas,Morogoro
PAMOJA na kuwepo kwa Sheria, Sera na Mikakati inayosisitiza ustawi wa wenye mahitaji maalumu bado Vituo na Vyuo vya ufundi stadi kumekuwa hakuna haki usawa ya elimu ya ufundi stadi kwa vijana wenye ulemevu wa akili.
Aidha, inaelezwa kuwa fursa za mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wenye ulemavu wa akili zimekosekana kwenye vyuo na vituo hivyo na changamoto kubwa iliyopo ni kutokana na kukosekana kwa mitaala mahususi.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Vijana na Wanawake Mafiga (MWAYODEO) Mkoani Morogoro, Venance Mlali alieleza hayo wakati wa mafunzo kazini ya siku tano kwa Walimu wa Vituo na Vyuo vya ufundi stadi Manispaa ya Morogoro, kwamba mafunzo hayo ni matokeo ya mradi wa kuleta mabadiliko kwa kutoa fursa za ufundi stadi kwa vijana wenye ulemavu wa akili Tanzania (PROYOUTH) kwa ufadhili wa Shirika la VAASA Association For Developing Countries (VADC) la nchini Finland.
Mlali alisema kupata mafunzo kwa walimu hao kutawawezesha kuwa na weledi na stadi za ufundi zaidi na lengo ni kukuza maisha bora ya watu wenye ulemavu wa akili ili kuleta mabadiliko endelevu, utoaji wa elimu, hamasa na uhamasishaji kwa jamii.
“Zipo sera na mikakati inayosisitiza ustawi wa wenye mahitaji maalum, kwa ujumla hali na ustawi kwa kundi hili kwa Tanzania si nzuri, na vyuo vya Ualimu wa Ufundi stadi havitoi kozi kwa walimu wa ufundi stadi hivyo kupitia mtadi huu wa PROYOUTH tunaendelea kuwawezesha wenye mahitaji na walimu waliopo kwenye vyuo,”alisemaa.
Aidha alisema mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi Tanzania ya mwaka 2009 hadi 2017 umeeleza namna mfumo wa elimu ambao watoto, vijana na watu wazima wanavyotakiwa kushiriki kikamilifu na kufikia malengo yao ya elimu kwenye shule na program nyingine zaelimu pasipo kujali hali na uwezo wao.
Pia alisema mradi huo umelenga kuwafikia vijana wenye ulemavu wa akili 150 wasichana wakiwa 70, mpaka sasa vijana 90 wamefikiwa na mradi huo ni wa miaka minne umeanza mwaka 2019 na utakamilika mwaka 2022 huku fedha zilizotolewa ni Euro 200,000 sawa na shilinhi 500 milioni, na kwamba kiasi kikubwa kinaenda ada ada vyuoni.
Aliiomba Serikali kuona namna ya kuweza kuwasaidia wenye ulemavu wa akili kulingana na uwezo wao(kiwango chao) na uwezo wa kujiunga kwenye vikundi upon a tayari wapo vijana wenye ulemavu wa akili wamejifunza ufugaji wa kuku, ufyatuaji matofali na useremala, halmashauri ziangalia ni kwa namna gani wanaweza kutengewa maeneo kama vitalu vya miti.
Mwalimu kutoka chuo cha Ualimu wa mafunzo ya Ufundi stadi Veta(VTTC) Morogoro Deogratias Ilembo alisema kuna haja ya vyuo vya ufundi nchini kuwa na mwongozo ama utaratibu maalumu kwa ajili ya elimu jumuishi kwa vijana wenye ulemavu wa akili kwani kwa kufanya hivyo wanaweza wakawa na uwezo wa haali ya juu.
Ilembo alisema wazazi na walezi wanatakiwa kuwa na fikra zaidi juu ya watoto wao badala ya kuwafungia ndani na kuwaona kuwa hawawezi lolote jambo ambalo si sahihi na endapo vijana hao wenye ulemavu wa akili wakiwezeshwa na kuchanganyika na watu wengine wanauwezo wa kuwa ma mabadiliko.
Vyuo vinayopokea Vijana hao ni Nongwa FDC, VETA Kihonda, Chuo ya Teknolojia ya ujenzi, Social Education Center, MOECO na MIHAYO.
No comments:
Post a Comment