Breaking News

Oct 22, 2021

WALIMU 'WAPIGANA MSASA' ELIMU YA UONGOZI MAHALI PA KAZI

   


WALIMU 'WAPIGANA MSASA' ELIMU YA UONGOZI MAHALI PA KAZI

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

CHAMA cha Walimu Manispaa ya Morogoro(CWT) kimeendesha mafunzo kwa kwa makatibu tawi ambao ni wawakilishi mahala pa kazi katika shule wanakofundisha wametakiwa kuzingatia sheria,kanuni na miongozo katika utatuzi wa migogoro mbalimbali inapoibuka katika maeneo yao ya kazi.

Wito huo, umetolewa na Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Morogoro,Jumanne Nyakirang’ani wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa makatibu wa matawi CWT Manispaa ya Morogoro na kuongeza kuwa kiongozi anapaswa kuwa na uadilifu na uweledi wa juu katika kusikiliza changamoto za watu katika maeneo ya kazi na kuzipatia ufumbuzi.

“Niwaombe viongozi wote kuhakikisha ya kuwa mnaingaza vema chama cha walimu (CWT) katika maeneo yenu ya kazi na kuwashawishi walimu ambao hawajajiunga na chama ili waweze kujiunga na kuleta mshikamano imara”Alisema Nyakirang’ani.

Awali,Mwenyekiti wa CWT manispaa ya Morogoro,Gaspar Jaka alisema kuwa mafunzo hayo kwa makatibu wa matawi na wawakilishi wa mahala pa kazi wanayopatiwa viongozi katika eneo lake utawala ni utaratibu wa kawaida katika kalenda ya kazi ya chama katika kuwajengea viongozi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Jaka alisema kuwa kupitia mafunzo yao yatapunguza changamoto zinawakuta walimu wanapotekeleza majukumu yao ili kuleta ufanisi mkubwa kitaasisi na kuinyanyua taaluma kwa wanafunzi.

Mwakilishi wa walimu mahala pa kazi kutoka shule ya msingi Mafisa B Manispaa ya Morogoro,Benadetha Mkasi alisema moja ya changamoto ni upandaji wa madaraja kwa walimu na masilahi hivyo kupitia mafunzo hayo yatasaidia kukabiliana changamoto hizo kwa kufuatilia katika mamlaka husika.

George Lukoa ni Katibu wa CWT manispaa ya Morogoro alisema mafunzo hayo kwake yatakuwa ni chanju ya mabadiliko ya uwajibikaji katika maeneo ya kazi ili kuleta matokeo yenye tija na kuachana na dhana ya kufanyakazi kwa mazoea.

No comments:

Post a Comment