OCODE
YAJENGA DARASA LA AWALI SHULE YA MSINGI MALAMBA
NA VICTOR MASANGU
KATIKA kuendelea kuunnga
mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu
kuanzia ngazi za msingi hadi sekondari hapa nchini Shirika la kitaifa
lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE)
limefanikiwa kujenda chumba kimoja cha darasa la awali katika shule ya msingi
Malamba mawili ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 27.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo la Ocode Joseph
Jackson wakati wa sherehe za makabidhiano ya chumba hicho cha darasa la awali
ambapo iliambatana na halfa ya kuwakabidhi tuzo kwa walimu bora wanne ambao
wameweza kujituma na kufanikiwa kufanya vizuri katika ufundishaji na
ujifunzaji.
Katika halfa hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya
shule ya msingi Malamba mawili mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, walimu wakuu kutoka baadhi
ya shule zilizopo katika manispaa ya ubungo sambamba na maafisa elimu wa
shule za msingi na wanafunzi.
Mkurugenzi
huyo katika Hotuba yake kwa mgeni rasmi alibainisha kwamab shirika hilo
lilianzishwa tangu mwaka 1999 na kupata usajili wake mnamo mwaka 2003 na kwamba
linafanya kazi zake kwa ajili ya kuisaidia jamii pamoja na kuboresha maisha ya
watanzania ambao wanaishi katika hali duni na wale wenye mahitaji maalumu.
Alisema kwamba wameamua kujenga chumba hicho cha darasa moja kwa
ajili ya wanafunzi wa awali kwa lengo la kuweza kuwasaidia katika kupata elimu
bora na kwamba shirika lao tangu mwaka 2019 hadi mwaka huu tayari limefanikiwa
kusaidia katika sekta ya elimu kwa shule mbali mbali ikiwemo kujenga madarasa
mawili katika shule ya msingi Kibwegere, pamoja na Goba na kwamba jumla
yanakuwa madarasa matatu.
Pamoja
na ujenzi wa madarasa hayo Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa katika madarasa
hayo wameweza kuweka mdawati yapatayo 30 katika kila shule ulipopita
mradi huo, ikiwemo viti 12 pamoja na kupeleka meza tatu katika shule ya msingi
Malambamawili.
“Kwa kweli shirika letu la Ocode katika mradi huu ambao
tunauendesha katika manispaa ya Ubungo tumeweza kushirikiana bega kwa began a
idara ya elimu na uongozi wa manispaa ya Ubungo kwa kweli wanatupa sapoti kubwa
na licha ya hayo yote tumeweza kutoa mafunzo mbali mbali kwa walimu wetu wa
shule za awali,pamoja na wale wanaofundisha darasa la kwanza hadi la tatu lengo
ikiwa ni kuboresha mbinu za ufundishaji zaidi,”alifafanua Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Herry James ambaye
ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo ameupongeza uongozi wa shirika la
Ocode kwa kuweza kutoa mchango wake wa kuboresha sekta ya elimu pamoja na kuona
umuhimu wa kuwathamini na kuwajali watoto wenye ulemavu kwa kuwatengenezea
miundombinu ambayo ni rafiki.
“Jamani
hawa walimu inatakiwa tuangalie jinsi ya kuishi na hawa walimu maana ni watu
muhimu sana katika taifa letu hili la Tanzania, maana wakija kuamua kufundisha
mambo ambayo sio mazuri hivyo siis kama serikali tutahakikisha jambo hli la
walimu tunaliztilia mkazo ili waweze kufundisha kwa weledi ambao unastahili, “alifafanua
mkuu huyo wa Wilaya.
Aliongeza
kuwa wao kama serikali watahakikisha kwamba wanaendelea kuboresha zaidi
mazingira ya walimu kwa kuwalinda na kuwajengea misingi bora ambayo itawasaidia
katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwafundisha wanafunzi na
kuhakikisha wanatoa malezi mazuri ambayo yatakuwa ni msaada wa kulisaidia Taifa
katika siku za mbeleni.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba ataendelea kushirikiana bega
kwa began a shirika hilo la Ocode kwa kazi zote ambazo zinazifanya katika
Nyanja mbali mabli na kuwahimza kuendelea kushirikiana na serikali katika kila
jambo kwa manufaa ya wananchi ya kuleta chachu ya maendeleo kwa ujumla.
Kwa upande wake Afisa elimu msingi katika Manispaa ya Ubungo
Abdul Buhety alibainisha kwamba ujenzi wa chumba hicho cha darasa la awali
katika shule ya msingi Malamba mawili kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa
wanafunzi kuweza kupata fursa ya kupata elimu na kujifunza mambo mbali mbali.
“Idadi
ya wanafunzi kila mwaka inazidi kuongezeka nah ii yote ni kutokana na kuwepo
kwa elimu bila malipo kwa hiyo uwepo wa ujenzi huu wa darasa la watoto wetu
ngazi ya awali amabalo limejengwa na shirika la Ocode kwetu sisi ni hatua nzuri
ya kuwasaidia watoto wetu wawez e kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwa
hiyo tuwapongeze sana wenzetu kwa juhudi za kuboresha sekta ya elimu,”alisema.
SHIRIKA la kitaifa lisilokuwa la kiserikali la Organization for
Community Devolopment tangu kuanzishwa kwake rasmi manamo mwaka 1999 limeweza
kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo ya kuisaidia jamii katika
Nyanja mbali mbali hususan katika sekta ya elimu ambapo imejenga
madarasa, pamoja na kusaidia madaati,viti pamoja na meza za walimu shule
mbali mbali.
No comments:
Post a Comment