Diwani wa Kata ya Visiga Mbugu Legeza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na ujenzi wa zahanati hiyo.
Wananchi wa Visiga Kibaha wahaidiwa neema huduma ya afya
VICTOR MASANGU, KIBAHA
WANANCHI wa
mtaa wa miwaleni uliopo Kata ya Visiga katika Halmashauri ya mji wa Kibaha
mkoani Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa
huduma ya afya kwa kipindi cha zaidi ya miaka 55 hatimaye wanatarajia
kuondokana na kutembea umbali wa kilometa 15 kwa ajili kufuata huduma ya
matibabu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa zahanati mpya.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Visiga Mbegu
Legeza kwa niaba ya wananchi wake wakati wa hafla ya makabidhiano ya
jengo la zahanati hiyo iliyojengwa kwa ufadhili wa
Taasisi ya Kiiislam ya Al- Swadiq Al-Ameen Foundation kwa ajili ya
kuikabidhi rasmi kwa uongozi wa serikali ya halmashauri ya mji
Kibaha ili iweze kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wa kata ya Visiga
na maeneo mengine ya jirani .
Diwani huyo alibainisha zahanati hiyo ambayo imejengwa katika
mtaa wa miwaleni itasaidia kuwapunguzia kero na adha kubwa ambayo walikuwa
wanaipata wananchi katika kipindi cha miaka ya nyuma kutokana na kutembea
umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kufuata huduma ya matibabu katika maeneo ya
mbali.
Aliongeza kuwa ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuunga mkono juhudi
za serikali katika kusaidia kuboresha sekta ya afya hasa kwa wananchi ambao
wananchi katika maeneo ya pembezoni na kwamba mradi huo utaweza kuzinufaisha
kaya zaidi ya 400 katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya matibabu.
“Mimi kama Diwani wa kata hii pamoja na Afisa mtendaji wangu wa
kata pamoja na wananchi kwa ujumla tumefarijika sana kwa ujio wa zahanati hii
maana ni zaidi ya miaka 50 sasa wananchi hawa katika mtaaa huu walikuwa hawana
huduma ya zahanati kwa hiyo hii taasisi imeweza kufanya jambo la muhimu sana
katika kuisaidia jamii ambayo inatuzunguka na sisi tunaendelea kushirikiana
nao,”alisema Diwani huyu.
Kwa upande wake kiongozi wa taasisi hiyo Shekh Said Chega
amesema kwamab wameamua kujenga mradi wa zahanati katika eneo hilo kutokana na
kuguswa na kubaini kuwepo kwa changamoto za huduma ya upatikanaji wa matibabu
kwa wananchi wa mtaa huo kwa kutumia muda mwingi kwenda kutibiwa katika maeneo
ya mbali.
Pia kiongozi huyo alifafanua kwamba lengo lao kubwa ni
kuhakikisha kwamba wanashirikiana naa serikjali katika kuanzisha miradi mbali
mbali ya kimaendeleo lengo ikiwa ni kuwasaidia wananchi ambao wanakabiliwa na
changamoto mbali mbali zinazowakabili katika Nyanja mbali mbali na kuweza
kuzitafutia ufumbuzi.
“Taasisi yetu inashughulika na mambo mbali mbali hasa katika
kusaidia jamii ambayo inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika sekta ya
afya, elimu, maji na mambo mengine yanayohitajika kwa hivyo sisi tulibaini
uwepo kwa wananchi wa mtaa huu kusumbuka katika huduma ya afya na ndio maana
tukaamua kujenha zahanati hii ambayo imegharimu kiasi cha shilingi milioni
70,”alisma kiongozi huyo.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Kibaha
akipokea jengo hilo la zahanati kwa niaba ya serikali amebainisha
kuwa mradi huo utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi na kuwataka kuhakikisha
wanailinda miundombinu yote na kuachana kabisa na vitendo vya kufanya hujuma na
wizi wa vifaa mbali mbali katika zahanati hiyo kwani imejengwa kwa ajili yao.
Afisa mtendaji wa kata ya Visiga Aloisia Nyello akusita kutoa
pongezi zake za dhati kwa uongozi mzima wa Taasii hiyo na kubainisha kwamba
mradi huo wa zahanati ni moja ya hatua kubwa katika kuwasogezea huduma wananchi
ya matibabu na kwamba mpaka kukamili kwake umegharimu kiasi cha shilingi
milioni 70 na utaweza kuwasaidia wwakazi wa maendeo mbali mbali.
Kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa zahanati ya mtaa wa
Miwaleni iliyopo kata ya Visiga Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kutaweza
kuwaondolea changamoto ya wananchi kutembea umbari wa kilometa 15
pamoja na kuzisaidia kaya zaidi ya 400 kupata huduma ya matibabu kwa uhakika
zaidi
No comments:
Post a Comment