Dr. Joyce Kahembe kutoka TIE akichangia hoja katika
maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike.
WADAU WAKUTANA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE
NA VICTOR MASANGU
KATIKA
kuadhimisha siku ya mtoto wa kike Kitaifa mashirika mbali mbali hapa nchini
yameungana kwa pamoja kwa lengo la kuweza kusherekea siku hiyo ikiwe kwa
kufanya shughuli za kimaendeleo sambamba na kukutana na wadau kwa lengo la
kuweka mikakati na kujadili mipango ambayo itamsaidia mtoto wa kike kukabiliana
na changamoto mbalimbali zinazomkabili.
Moja ya mipango ambayo imezungumziwa katika siku hiyo
maadhimisho ni pamoja na kuhakikisha kunatengenezwa mifumo imara ya kumwezesha
mtoto wa kike kupatiwa stadi za maisha kuanzia ngazi za chini ambazo zitaweza
kumsaidia kwa kiasi kikubwa katika kujitambua na kuelewa mambo mbalimbali
ambayo anastahili kuyapata ikiwemo kupatiwa haki zake za msingi.
Kwa kuliona hilo Shirika lisilokuwa la kiserikali la Regional
Educational Learning Initiative (RELI) kwa kushirikiana na wadau wengine
mbali mbali wa maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030 limekuja na
mpango madhubuti kwa ajili ya kuweza kushughulikia changamoto mbali mbali
zilizopo katika sekta ya elimu kwa kuja na mfumo ambao utaweza kusaidia
wanafunzi kupatiwa stadi za maisha na hatimaye kufanya kazi wenyewe kwa karne
ya 21.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa upimaji wa stadi za maisha
Afrika mashariki (ALIVE) Samsoni Sitta amebainisha kwamba Kongani yao kubwa
waliyojiwekea katika mradi huo ni kuhakikisha wanamsaidia mtoto wa kike ili
aweze kujitambua pamoja na kujifunza mambo mbali mbali anayokutana nayo katika
maisha yake .
“Lengo kubwa la mradi huu ni kuwasaidia wanafunzi wetu
katika suala zima la stadi za maisha na kitu kingine kikubwa ambacho
tunakiangalia ni hawa watoto wetu wa kike ambao bado wapo shuleni wanasoma
waweze kufanikiwa katika maisha yao katika siku zijazo ikiwa sambamba na
kutimiza malengo ambayo wamejiwekea kwa hiyo mimi kama mtaratibu nitahakikisha
mambo haya ya msingi yanafanikiwa,”alisema Mratibu huyo.
Aidha, katika hatua nyingine mratibu huyo aliongeza kuwa kuna
mambo makuu matatu ambayo ana imani yakisimamia na kufanyiwa utekelezaji
wake kwa nguvu zote kutaweza kumtegenezea kijana mbinu za kuweza kufika
mbali zaidi kupitia elimu ya stadi za maisha kwa kushirikiana na wadau mbali
mbali ikiwemo na viongozi wa serikali.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya haki elimu, Richard
Mabala alisema kuwa wataendelea kushirikiana kwa hali namali na wadu
wengine wa maendeleo pamoja na serikali kwa lengo la kuwasaidia watoto wa
kike kuweza kufundishwa mambo mbali mbali pindi wanapokuwa nyumbani pamoja na
shuleni masuala mazima ya stadi za maisha ambayo itawasaidia kupambana na maisha.
“Jambo la msingi kwa watoto wetu wa kike kuwapatia stadi za
maisha kwani naweza kusema kwamba na kutolea mfano kijiko kimoja cha sukari
kwenye birika zima la chai hauwezi kupata ladha ya chai kabisa na uchopekaji wa
stadi za maisha na kwamba baadhi ya mambo Fulani Fulani hivi kama vile baioloji
na uraia haiwezi kutosha kuwajengea watoto umahiri katika jambo la stadi za
maisha.”alisema Mabala.
Naye mmoja wa wanafunzi anayesoma kidato cha pili katika shule
ya sekondari Bundikani iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, Sifa Mapinduzi
ameiomba serikali ya awamu ya sita iweke mpango wa kuona umuhimu wa stadi za
maisha kuwa kama somo rasmi linalofundishwa darasani ili kuwaongezea
uelewa zaidi watoto wa kike katika suala zima la kujielewa pamoja na kujitambua.
“Serikali sasa kutokana na umuhimu wa stadi za maidha inatakiwa
sasa liingizwe rasmi kama somo ambalo litakuwa linafundishwa darasani,kwa sababu
mimi baada ya kujifunza stadi za maisha kumeweza kunisaidia kwa kiwango kikubwa
katika kujiamini na hata leo ndio maana naonge na nyie viongozi na watu wa
kubwa nina jiamini kweli,”alisema Mwanafunzi huyo.
Kwa upande wake, Dr. Joyce Kahembe kutoka TIE alibainisha kwamba
stadi za maisha zimeweza kuchopekwa katika masomo ya biology pamoja na
pamoja na somo la uraia lengo ikiwa ni kuwasaidi watoto wa kike kupambana na
changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika maisha yao hivyo ni jambo
ambalo linatakiwa kutiliwa mkazo zaidi.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani kwa mwaka huu
wa 2021 yamefanyika kwa mafanikio makubwa kupitia muunganiko wa
baadhi ya mashirika mbalimbali yakiwemo RELI,kupitia
mradi wake wa (ALIVE) pamoja na Room to Read huku kauli mbinu yake
inasema kuwa stadi za maisha ni ufunguo wa ndoto za mtoto wa kike.
No comments:
Post a Comment