KIWANGO CHA UFAULU MASOMO YA SAYANSI WANAFUNZI WA KIKE SUA CHAONGEZEKA
Na Thadei Hafigwa
IMELEZWA kuwa kiwango cha ufaulu katika masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa kike kimeongezeka ikilinganishwa na wanafunzi wa kiume katika chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo,kilichopo Mkoani Morogoro,kutokana na mwamko kwa wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sanyansi
Dk.Nyambilila Amuri,Mkurugenzi shahada za awali,Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) alibainisha yao wakati akiongea na waandishi wa habari chuo hapo na kuongeza kuwa mwamko wa ufaulu umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuwepo kwa sera ya usawa wa jinsia katika udahili kwa wanafunzi katika kujiunga na chuo hicho.
Dk.Amuri alisema uwiano uliopo katika kujiunga na chuo hicho ni asilimia 60 kwa wanafunzi wa kiume na asilimia 40 ni wanafunzi wa kike lakini katika kipindi cha masomo yao wanafunzi wa kike wanaochukua fani mbalimbali za sayansi wamekuwa wakionesha ufaulu mkubwa ukiringanisha na wanafunzi wa kiume.
“Nitoe wito wa jamii kwamba kuendelea kuwaamini mtoto wa kike kwamba anauwezo mkubwa wa kufaulu masomo ya sayansi iwapo wakipewa fursa,hivyo ni jukumu la kila mwanajamii kuhakikisha watoto wote wa kike na wa kiume wana fursa sawa ya kupata elimu ya juu hasa kwa masomo ya sayansi.
Aidha,kutokana na ufaulu kwa wanafunzi wa kike katika masomo ya sayansi,uongozi wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) wamefikia uamuzi wa kuwatunuku tuzo kwa wanafunzi hao zaidi ya wanafunzi 60 waliofanya vizuri ukiringanisha wanafunzi wa kiume waliohitimu katika ngazi mbalimbali za elimu katika masomo ya sayansi.
Uamuzi huo wa menejimenti ya SUA imelenga zaidi kuongeza hamasa kwa wanafunzi kusoma zaidi masomo ya sayansi kwa bidii kubwa ili kuleta machango mkubwa wa kuboresha uchumi wa nchi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment