Zahanati ya Viziwaziwa Kibaha kupewa hadhi kituo cha afya
Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala la changamoto ya afya kwa wananchi wa kata ya viziwaziwa kwa kuweka mipango ya kuanzisha mradi wa kituo cha afya.
Koka ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa wananchi wa kata ya Sagare katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili katika sekta mbalimbali.
Aidha, Mbunge hiyo aliongeza kuwa anatambua kuwa katika kata ya viziwaziwa kuna uhitaji wa huduma za afya licha ya uwepo wa zahanati lakini katika kuongeza huduma ya afya kwa wananchi kuna kila sababu ya kujenga kituo cha afya ili kuondokana na adha ya kufuata huduma ya matibabu katika maeneo ya mbali.
"Kwa Sasa na tambua kuna zahanati moja katika kata hii ya viziwaziwa lakini kitu kikubwa ni kuipandisha hadhi zahanati yetu ili iweze kuwa kituo cha afya na nina imani itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero,"akisema Koka.
Pia, Koka alisema katika kuwaboreshea huduma ya matibabu hususan kwa wakinamama wajawazito kwa kuanzisha mradi wa ujenzi wa wodi kwa ajili ya kujifungulia.
Katika hatua nyingine Koka amechangia kiasi Cha shilingi milioni Mbili kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule ya msingi ili kuweza kuwasaidia wanafunzi kutotembea umbari mrefu.
"Kutokana na umuhimu wa elimu na watoto wetu kutembea umbali mrefu mimi nachangia kiasi cha shilingi milioni mbili ambazo zitaweza kusaidia katika ujenzi huo wa mradi wa shule ya msingi,"alisema Koka.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya viziwaziwa, Mudy Mussa alitoa pongezi kwa Mbunge huyo kwa kufanya ziara ya kwenda kusikiliza kero za wananchi licha ya kukabiliaa na baadhi ya changamoto.
Diwani huyo alisema kwa sasa
wanakabiliwa na changamoto ya huduma ya nishati ya umeme,afya pamoja na shule
hivyo kunahitajika nguvu za makusudi ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
No comments:
Post a Comment