Breaking News

Sep 24, 2021

KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MOROGORO WAMEPONGEZWA NA NHIF

KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MOROGORO WAMEPONGEZWA NA NHIF

Na Mwandishi wetu,Dodoma

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Umetoa cheti cha kutambua mchango wa waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro kwa namna inavyoshirikiana na mfuko huo katika kuandika habari zake na kuhamasisha jamii kujikinga na mfuko huo.

Katibu Mtendaji wa Morogoro Press Club,Lilian Lucas mara baada ya kupokea cheti hicho,ameshukuru uongozi wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa hatua hiyo ya kutambua mchango wa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro kwa jitihada zao

Lilian amesema kwa kipindi kirefu Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro kupitia chama cha waandishi wa habari mkoani hapa(MOROPC) wamekuwa na mahusiano mazuri kikazi na mfuko wa taifa ya bima ya afya (NHIF) na kwamba wataendelea kuimarisha mahusiano hayo.

“Tunaushukuru uongozi wa NHF kwa kutambua mchango wa wanahabari,nami kwa niaba ya uongozi wa Morogoro Press Club ninataka kuwahakikishia ya kuwa mahusiano yetu yataendelea kudumishwa na wategemee kazi nzuri yenye uweledi kutoka kwetu”alisema katibu huyo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mapema leo.

Hafla ya utoaji wa cheti hicho ilifanyika Septemba 24,2021 Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 toka kuanzishwa kwa mfumo wa NHIF na kuwakutanisha waandishi wandamizi kutoka mikoa yote hapa nchini.

No comments:

Post a Comment