MKURUGENZI MTENDAJI,HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE,MUSSA GAMA
HALMASHAURI
KISARAWE YATENGA BIL.39.8 MIRADI YA MAENDELEO
NA
VICTOR MASANGU, KISARAWE
BARAZA la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya
Kisarawe mkoani Pwani limeazimia kwa pamoja kupitisha bajeti ya kiasi cha
shillingi bilioni 39.8 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango
wake wa matumizi katika sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo kwa
kipindi cha mwaka 2021 na 2022.
Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe, Mussa Gama wakati wa kikao cha baraza hilo kwa ajili ya
kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti hiyo kilichohidhuriwa na viongozi
mbali mbali wa serikali, Taasisi za umma, wakuu wa idara pamoja na wakuu
wa vitengo kutoka mashirika ya umma ambao walialikwa lengo la kutoa elimu kwa
madiwani hao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate
Mwegele amewaasa madiwani kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii
na weledi ikiwemo kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na
kuitifatua ufumbuzi lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo
katika sekta mbali mbali.
Pia,Jokate alisema kwamba serikali ya Wilaya ya Kisarawe,
itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa madiwani wote na watendaji
bila ubaguzi wowote kwa lengo la kuweza kuwaletea wananchi maendeleo
katika nyaja bali mbali za maji, umeme afya, na mambo mengine
ya msingi kwa kuzingiatia miongozo,taratibu na sheria zote zilizowekwa za
nchi.
Naye, Mwenyekti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,
Halfan Sika amelipongeza baraza hilo la madiwani kwa kuweza kushikamana kwa
pamoja na kupitisha bajeti hiyo ambayo inakwenda kutatua au kupunguza
kero na shida mbalimbali za wananchi wa maeneo mbalimbali ya Kisarawe.
Sika aliongeza kuwa, lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni
kuhakikisha kwamba inaleta maendeleo kwa wananchi wake kwa kuzingatia
utakelezaji wa ilani ya chama katika yale mambo mbalimbali ambayo
yameahidiwa ili yaweze kufanyiwa kazi na kuleta mabadiliko katika Nyanja mbalimbali.
“Mimi niwapongeza madiwani wote ambao kwa kweli mmeweza kufanya
kazi kwa bidii katika kuiandaa bajeti hii na kitu kikubwa ambacho tunapaswa
kukifanya ni kuhakikisha tunaweka mipango yetu vizuri ya kuweza kuwatumikia
wananchi wetu ikiwemo kuwatatulia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili na
kuzitafutia majawabu kwa hivyo nina imani kupita kwa bajeti hii ni moja
kati ya hatua katika maendeleo kwa wanachi wa Kisarawe.”alifafanua Sika.
Nao, baadhi ya madiwani wa baraza hilo akiwemo Adamu
Nimba na Mhandisi Mohamed Kilumbi, wameoumba uongozi wa halmashauri
hiyo ya Kisarawe licha ya kupisha bajeti hiyo lakini waongeze ubunifu zaidi
katika suala zima la ukusanyaji wa mapato kwa kuwa ni vyanzo vingine vipya
ambayo vitaweza kuisaidia kuinua kiwango cha mapato.
“Sisi kama baraza la madiwani hii bajeti tumeipitisha
lakini kitu kikubwa ni lazima kujipanga zaidi na kuwatumia wataalamu wetu wa
Kisarawe ambao wataweza kuzidisha kazi zaidi katika suala zima la ukusanyaji wa
mapato ya ndani kwa kupitia njia mbalimbali za kubuni vyavyo vipya vya
muda mrefu katika ukusanyaji wa mapato hayo,”alisisitiza Adamu.
Kadhalika, Diwani huyo katika hatua nyingine, alifafanua
kwamba vyanzo vya mkaa na kuni ambavyo navyo vinatumika katika ukusanyaji
mzima wa kuingiza kipato lakini vitafikia wakati vitakwisha hivyo kunapaswa
kuwekwa mpango endelevu ambao utasaidia katika siku za usoni kupata suala la
upatikanaji wa kuingiza mapato.
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ni miongozi mwa halmashauri
tisa zilizopo katika Mkoa wa Pwani ilianzishwa mwezi Agosti mwaka
1962,ambapo kwa mwaka huu upitishwaji wa bajeti hiyo itaweza kwenda kuleta
mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kupunguza changamoto za ukosefu wa
huduma mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabiliwa wananchi katika maeneo
yao.
No comments:
Post a Comment