Zao la Korosho nchini Tanzania
Na Mwandishi wetu
Tanzania imeshika nafasi ya nne katika uzalishaji wa Kilimo cha korosho huku nchi za Ivory Coast na Nigeria,zikiongoza katika kuzalisha zao hilo Afrika na Duniani.
Kasiga Ngila Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI), Kituo cha Naliendele kitengo cha Agronomia ya Korosho, amewaeleza wakulima wa korosho kutoka Halmashauri za Kilosa na Gairo mkoani Morogoro kwamba Tanzania imekuwa ni nje ya mfano kwa kutoa elimu katika uendelezaji wa zao la Korosho.
Ngaila akinukuu takwimu ambazo zimepatikana kutoka mtandao wa Kilimo forum.com zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya nne barani Afrika kwa kuzalisha korosho ikitanguliwa na Nigeria inayoongoza kwa kuzalisha tani za ujazo laki tisa kwa mwaka ikifuatiwa na Ivory Coast inayozalisha tani za ujazo laki sita.
“Takwimu hizo imetupa changamoto kwetu nchi zinazoongoza kwenye uzalishaji kwa wingi kuliko sisi, tuliwafundisha wao wamekuwa wepesi kuchangamkia fursa hiyo,sasa wamekuwa vidara katika zao hilo,wakulima wetu bado wanahitaji kupewa hamasa, ndio maana sasa tumeamua kusambaza elimu kwa wakulima wetu ili na sisi tuongeze uzalishaji,” alisema Kasiga.
Ametaja nchi ya tatu kwa kuzalisha Korosho barani Afrika ni Guinea Bissau inayozalisha tani za ujazo laki nne kwa mwaka ambapo Tanzania inazalisha tani za ujazo laki tatu kwa mwaka.
Kasiga amesema kuwa kwa Duniani nchi
inayoongoza ni Vetnam ikizalisha tani za ujazo milioni 1.2 ya pili ikiwa ni
Nigeria ikizalisha tani laki tisa,India ikizalisha tani laki tisa na Ivory
Coast tani laki sita.
Mtafiti wa Magonjwa na Visumbufu vya zao la Korosho Dk Wilson Nene,alisema sababu inayopelekea kuwepo kwa uzalishaji mdogo wa zao hilo hapa nchini ni pamoja na wakulima kushindwa kutumia mbegu bora za kisasa na badala yake wamekuwa wakitumia mbegu za kienyeji.
Sababu nyingi ni pamoja na wakulima kushindwa
kutumia viuatilifu vya kudhibiti visumbufu vya zao la korosho kwa wakati na
kuzingatia masharti yaliyowekwa hali ambayo imekuwa ikichangia kushindwa
kupandisha uzalishaji wa zao la korosho hapa nchini.
Dk Nene amesema tayari wameanza kuwafundisha wakulima kuanza kutumia mbegu bora za kisasa aina 54 zinazozalishwa na TARI Naliendele zenye uwezo wa kuzalisha mti mmoja zaidi ya kilo 20 tofauti na mbegu za kienyeji zinazotoa kilo 11.
No comments:
Post a Comment