Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,Bw.Crispian Francis Chalamila akitoa mada katika Kongamano la kimataifa.
TANZANIA inashiriki Kongamano la tano la Kimataifa la Mashirikiano katika Mapambano Dhidi ya Rushwa.
Kongamano hili ni mahususi kwa ajili ya Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa Duniani kubadilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na Rushwa.
Kongamano hili la siku tano, linahudhuriwa na Mamlaka 219 za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi 121 Duniani ikiwemo Tanzania ambapo - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanashiriki.
Pamoja na mambo mengine, Kongamano hili lilihusisha HIGH LEVEL FORUM (Warsha ya Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa) kutoa uzoefu wao wa namna Serikali zinavyofanikiwa kudhibiti Rushwa katika mataifa yao.
Maeneo yaliyozungumziwa ni pamoja na
1. GLOBAL VISION
2. MFUMO WA KISHERIA NA KITAASISI
3. UENDESHAJI WA GLOBE NETWORK NA
4. KUJENGA USHIRIKIANO
Kupitia Warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila ametoa uzoefu wa namna ambavyo Mfumo wa Sheria na Kitaasisi nchini Tanzania unawezesha Mapambano Dhidi ya Rushwa kufanikiwa.
Mkurugenzi Mkuu amesema Serikali ya Tanzania imekuwa ikipambana na Rushwa kwa kuimarisha mifumo ya sheria na ya kitaasisi ikiwemo kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama Kuu inayoshughulikia masuala ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Ameyasema hayo akiwasilisha mada kuhusu 'ANTI CORRUPTION AND INSTITUTIONAL LEGAL FRAME WORK IN TANZANIA' kwa Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanaoshiriki 'The 5th Global Operational Network of Anti Corruption Law Enforcement Authorities - GlobE Network'.
Kongamano hili linahudhuriwa na Mamlaka 219 za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi 121 Duniani - Tanzania ikiwa ni kati ya Nchi 70 zilizopewa fursa ya kutoa wasilisho.
Mtandao wa GlobE ulianzishwa 2021 kwa lengo la kubadilishana taarifa, uzoefu na utaalamu katika mapambano dhidi ya Rushwa na TAKUKURU ilijiunga na Mtandao huu Mwaka 2022.
KATIKA HATU NYINGINE, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, amemtembelea Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Khamis Mussa Omar Septemba 23, 2024 kwa lengo la kujitambulisha.
Akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu, Balozi Omar ameipongeza TAKUKURU kwa jitihada inazozifanya katika kuzuia na kupambana na rushwa na kuisisitiza TAKUKURU kutumia vema fursa ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na ya China kwani kuna mambo mengi ya kujifunza.
Mkurugenzi Mkuu yuko Beijing China kuhudhuria 'The 5th GlobE Network Meeting' inayofanyika Septemba 24 - 27, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine amewasilisha mada kuhusu *Mfumo wa Sheria wa Tanzania kwenye Mapambano dhidi ya Rushwa.*
No comments:
Post a Comment