Wenyeviti na Wasajili wa Mabaraza simamieni Maadili ya Wanataaluma - Waziri Ummy
Na. Mwandishi wetu (WAF)- Dodoma
Wenyevyiti na Wasajili wa
Mabaraza na Bodi za Kitaaluma nchini wametakiwa kusimamia maadili ya
wanataaluma ili kulinda jamii na huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Hayo yamesemwa leo na
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha pamoja na Wenyeviti wa
Mabaraza ya kitaaluma na Bodi za ujasili zilizo chini ya Wizara ya afya
kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri Ummy amesema
viongozi hao wanao wajibu mkubwa wa kusimamia Maadili ya wanataaluma ili
kuilinda jamii na huduma zinazotolewa kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma
zinatolewa kwa kiwango kinachofaa na ni salama.
"Serikali chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza katika miundombinu ya afya na kuboresha mazingira ya kutolea huduma pamoja na kutoa ajira kwa watoa huduma za afya kote nchini".
WAZIRI WA AFYA,MHE. UMMY MWALIMU(KATIKATI) AKIFAFANUA JAMBO KATIKA KIKAO KILICHOWAKUTANISHA WENYEVITI NA WASAJILI WA MABARAZA,JIJINI DODOMA"Kwa msingi huu mna nafasi kubwa sana ya kuisaidia Wizara
ya Afya katika kipaumbele kikubwa mwaka huu yaani kuongeza ubora wa huduma za
afya nchini". Alisisitiza Waziri Ummy.
Hata hivyo, Waziri Ummy
hakusita kuzungumzia malalamiko ambayo wananchi wamekua wakitoa kwa njia
mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, wananchi mmoja mmoja na kupitia mifumo ya
kutoa mrejesho wa Wizara ya Afya.
Ameongeza kuwa wananchi
wamekua wakielekeza malalamiko yao kwa wanataaluma mbalimbali juu ya huduma
mbaya, kukiuka Maadili ya kitaaluma na kutojaliwa wagonjwa na hata wanaotoa
huduma.
"Tumeshuhudia malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi kwenye vituo vya umma na hata kutoka kwenye hospitali binafsi, nawashukuru pale mlipofuatilia malalamiko hayo maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kubaini makosa na kuchukua hatua stahiki". Amesema Waziri Ummy.
WASHIRIKI WA KIKAO CHA PAMOJA KILICHOWASHIRIKISHAAidha, Waziri Ummy
aliwasisitiza wenyeviti na wasajili hao kutoa adhabu kali sana kwa wale
wachache wanaokaidi miiko na kanuni za maadili yao.
"Msiwaonee aibu,
malalamiko haya yanapozidi wananchi watakata tamaa na kuikosa imani kwa
Serikali yao ambayo imefanya juhudi kubwa kusogeza huduma za afya kwa wananchi".
Alisisitiza Waziri Ummy.
Aliongeza kuwa wananchi
wana haki ya kupata huduma bora, na kuwataka wanataaluma watambue hilo na
kutimiza wajibu wao kwa moyo wa upendo bila kusukumwa au kuona wanawatendea
hisani wateja wao.
"Mtoa huduma yeyote
awe kwenye vituo binafsi ama ya serikali
ana wajibu huu na wala sio hisani. Naagiza mkasimamie hili ili
wanataaluma waelewe na wapende kutimiza wajibu huu bila shuruti".
No comments:
Post a Comment